BREAKING NEWS|Tamisemi|Form Five Post Selection 2021|Majina Ya Waliochaguliwa Kidato Cha Tano 2021



The Minister of State, President's Office, Regional Administration and Local Government (Tamisemi), Ummy Mwalimu today Tuesday June Mosi, 2021 spoke to reporters in Dodoma.

 He said the number of students selected to join the fifth form for government schools and colleges of education and vocational training in 2021 has increased by 14 percent.

 The increase comes after the total number of candidates selected to join Form Five for Government schools and colleges of education and vocational training in 2021 to 148,127 from 129,854 in 2020.

 He said the election was based on the statistics of students who took the exam in 2020 from mainland Tanzania where the candidates who got first to third grade were 153,464 if 67,135 girls and 86,329 boys, equivalent to 35.06 percent of all candidates. He said in the case of independent candidates who completed Form Four in 2020 under the Institute of Adult Education who received first to third grade were 479 if 289 girls and 190 boys. 




Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Ummy Mwalimu leo Jumanne Juni Mosi, 2021 amezungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma. 

 Amesema Idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano kwa shule za Serikali na vyuo vya elimu na mafunzo ya ufundi mwaka 2021 imeongezeka kwa asilimia 14. 

 Ongezeko hilo linakuja baada ya jumla ya watahiniwa waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa shule za Serikali na vyuo vya elimu na mafunzo ya ufundi mwaka 2021 kufikia 148,127 kutoka 129,854 mwaka 2020.

 Alisema uchaguzi huo umefanyika kwa kuzingatia Takwimu za wanafunzi waliofanya mtihani mwaka 2020 kutoka Tanzania Bara ambapo watahiniwa waliopata daraja la kwanza hadi la tatu walikuwa 153,464 ikiwa wasichana 67,135 na wavulana 86,329, sawa na asilimia 35.06 ya watahiniwa wote. Alisema kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea waliomaliza kidato cha nne mwaka 2020 wakiwa chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ambao walipata daraja la kwanza hadi la tatu walikuwa 479 ikiwa wasichana ni 289 na wavulana 190.  








No comments